DigiByte ni chanzo -wazi cha blockchain kinachokua kwa haraka kilichoundwa mwishoni mwa mwaka 2013 na kutolewa mapema mwaka 2014. Baada ya miaka ya maendeleo ya ufikiriaji wa mbele, DigiByte imekuwa moja ya blockchain yenye usalama, kasi, ndefu na UTXO blockchain yenye madaraka.
Safu tatu ndizo sehemu kuu za uvumbuzi kwenye blockchain ya DigiByte zinazotoa miundombinu ya mtandao, ulinzi na mawasiliano katika ufanyaji kazi wa spidi ya ajabu.
Safu ya juu ni kama stoo ya programu iliyo na mwonekano na matumizi halisi ya dunia. Aina zote za mali za kigitail zinaweza kuundwa kupitia itikadi ya DigiAssets juu ya blockchain ya DigiByte. Programu zilizo na madaraka (dApps) zinaweza kuundwa juu ya blockchain ya DigiByte. Pia smart contracts zilizo ngumu na salama juu blockchain ya DigiByte zinaweza kuundwa kwa urahisi.
Safu/Tabaka la katikati hutoa usalama/ulinzi na utawala. Digital Byte ya data, huwakilisha data nyingi au kizio kinachoshikilia thamani na haiwezi kuwa bandia, kurudiwa au kufanyiwa utapeli. Kitabu/daftali la umma lenye ulinzi wa hali ya juu ambapo shughuli/miamala yote ya DigiByte inatunzwa. DigiByte inatumia algorithm tano kuthibitisha kazi kwa ajili ya ulinzi. DigiByte mpya hutokana na uchimbaji pekee.
Safu/Tabaka la chini hutoa mawasiliano na taratibu za ufanyaji kazi. Ni kiwango cha chini kabisa cha node kwenye DigiByte cha mawasiliano katika mtandao wa ulimwengu. Maelfu ya watu wanatumia programu ya DigiByte kote ulimwenguni. Seva, kompyuta, tablet au simu yoyote iliyounganishwa na mtandao wa DigiByte inakuwa node inayosaidia kupokea na kuruhusu miamala/shughuli. Anza kuchangia kwenye blockchain ya DigiByte kwa njia bora.
Kama ilivyo tovuti, DigiByte blockchain ni chanzo-wazi na kisicho na gharama kutumia kilichotolewa chini ya leseni ya MIT, ambacho kinakupa nguvu ya kuendesha na kubadilisha programu. Uwazi unaruhusu uthibitisho huru wa binary na chanzo cha misimbo/code zinazoendana.
Itifaki ya DigiByte kwenye GitHub.
Kiini cha maendeleo ya DigiByte kwenye GitHub.
Vumbua hatua muhimu za maendeleo makubwa ya blockchain ya DigiByte.
DigiByte (DGB) ni sarafu ya kidigitali ambayo inaweza kupanuka kutoka hatua moja kwenda nyingine na inawezesha kasi kubwa ya ufanyaji miamala kwa ada ndogo sana. DigiByte ni njia nzuri ya kufanya malipo.
Kuanza kutumia DigiByte ni rahisi zaidi kuliko hata kutuma meseji. Unaweza kutuma na kupokea DigiByte kwa kutumia vifaa ambavyo tayari unavijua na kuvipenda. Unachotakiwa ni kuweka Pochi inayopokea DigiByte kwenye kifaa chako alafu bonyeza scan, scan QR code na tuma DigiByte. Rahisi kama 1..2..3.
DigiByte haijawahi kufadhiliwa kupitia ICO au kiwango muhimu cha sarafu zilizochimbuliwa awali (0% iliyobaki). Hakuna Mkurugenzi Mtendaji au kampuni inayodhibiti DigiByte blockchain. Mwanzilishi, watengenezaji na jamii ni watu wanaojitolea wasio na malipo kitu ambacho kinaondoa hatari ya kufilisika.
Miamala ya DigiByte inathibitishwa ndani ya sekunde 15 kwa makadrio, ambayo ni mara 40 haraka zaidi ya Bitcoin na mara 10 haraka zaidi ya Litecoin. SegWit inawezesha mpaka miamala/shughuli 1066 kwenye mnyororo kwa sekunde na kwa ada ndogo sana kabisa na kuifanya DigiByte sarafu bora ya malipo ya kila siku.
DigiByte imeundwa kwenye teknolojia mahili ya blockchain ya Bitcoin na kuweka vitu mahili kabisa juu yake kama DigiShield guard, MultiAlgo mining na Odocrypt algorithm. Pia Dandelion++ privacy protocol inasaidia kukuweka salama kwa kuficha IP na eneo ulilopo. Jifunze zaidi.
DigiByte ni blockchain ambayo ni 100% Proof of Work (PoW) na inaweza kuchimbwa kwa algorithms 5 zinazoitwa Sha256, Scrypt, Skein, Qubit na Odocrypt. MultiAlgo mining inachangia madaraka (kutohodhiwa), usalama wa mtandao na kukupa uhuru wa kutumia vifaa tofauti kama ASIC, FPGA au GPU. Jifunze zaidi.
Ukilinganisha na Bitcoin milioni 21, DigiByte bilioni 21 (1000:1 kwa uwiano na BTC) zimetengenezwa tayari kwa ajili ya kupokelewa na watu wengi. DigiByte block rewards hupunguza 1% kila mwezi ya DigiByte zote badala ya kupunguza nusu ya block kila baada ya miaka 4. DigiBytes zote bilioni 21 zitakuwa zimechimbwa ifikapo mwaka 2035. Baada ya 2035 wachimbaji basi watategemea ada ya ununuzi peke yake. Jifunze zaidi.
Kubadilishana yote na huduma zote zinazowezesha DigiByte zinapatika kwenye DigiByte Wiki.
Kanusho la kubadilishana
Ofisi za kubadilishana yaliyoletwa hapa au kwenye CoinMarketCap ni kwa madhumuni ya habari tu na hayahusiani na jamii ya DigiByte. Ofisi yoyote ya kubadilishana inaweza kuorodhesha DigiByte bila ruhusa. Daima fanya utafiti wako mwenyewe kabla ya kuzitumia, kisha uhifadhi DGB yako katika pochi wa kibinafsi.
DigiAssets ni salama, safu ya juu yenye kuweza kupanuliwa ya blockchain ya DigiByte ambayo inawezesha utoaji madaraka ya mali/sarafu, smart contracts, digital identity na zaidi.
DigiAssets zinaweza kutumiwa kuwakilisha usalama wa kitu chochote tunachopata katika ulimwengu. Kutoka kwenye mali inayoonekana kama vile mali isiyohamishika au magari, kupitia kwa uhaba wa vipande vya sanaa vya kidigitali. Hati zilizosainiwa kama vile shughuli na bili za matibabu zinaweza kulindwa pia.
DigiAssets kama mfumo wa ikolojia na jukwaa tayari lina vyama vyenye nia ya kupanga au kujenga majukwaa katika mali zisizohamishika, fedha, malipo, utambulisho, sehemu ya kuuzia, mbio, biashara, huduma za afya, mnyororo wa usambazaji, serikali na zaidi.
DigiAssets inaleta huduma za kipekee za blockchain zilizoidhinishwa kupatikana ndani ya blockchain isiyo na ruhusa kama DigiByte. Hii inaruhusu DigiAssets kuwa salama zaidi, kupanuliwa na zisizoingiliwa na mtu yeyote kuliko jukwaa lingine lolote kwenye soko.
Vumbua chanzo-wazi cha vigezo vya itifaki ya DigiAssets kwa ajili ya kutoa na kufanya miamala ya mali/sarafu za kidigitali kwa kutumia blockchain ya DigiByte. Itifaki ya DigiAssets kwenye GitHub, Mabadiliko na upanuzi wa DigiAssets Core.
Sio mwana-programu? Kwa kweli sio shida! Mtu yeyote anaweza kutoa DigiAsset kwa urahisi kwa kutumia moja ya vifaa vinavyopatikana bila kuwa na ujuzi wa kiufundi juu ya itifaki. Huduma zinazoungwa mkono na DigiAssets.
Unajiuliza jinsi ya kutumia DigiAssets? Tembelea huduma zinazoungwa mkono na DigiAssets kununua, kuuza na kubadilisha DigiAssets.
Je, unahitaji msaada zaidi kuhusu DigiByte? Jisikie huru kujiunga na kundi la watengenezaji wa programu ya DigiByte kwenye Telegramu na uulize maswali yako au uwasilishe mchango wako wa kimawazo. Watengenezaji wa programu za DigiByte kwenye Telegramu.
Gundua huduma za DigiAssets zilizokubaliwa kupata uzoefu wa DigiAssets.
Digi-ID ni itikadi ya usalama iliyojengwa juu ya teknolojia ya blockchain ya DigiByte kuwezesha watumiaji kuweka jitihada kidogo kuingia kwenye tovuti, programu na zaidi.
Digi-ID inaondoa jina la mtumiaji, nenosiri na mahitaji ya uthibitisho wa 2fa. Kwa sababu Digi-ID hutumia kifunguo cha umma / kibinafsi cha faragha, hakuna manenosiri au majina ya watumiaji yaliyo hatarini. Njia hii sio tu inalinda watumiaji, inalinda pia huduma ambazo mtumiaji hutumia.
Digi-ID hahifadhi taarifa yoyote kuhusu watumiaji kwenye blockchain. Hii inaimarisha usalama na pia inazidisha ujasiri wa watumiaji wa mwisho kwamba taarifa zao hazifuatwi wala kuwa kwenye hatari kwa uzembe wa wengine. Hakuna hatua ya nje ya kutofaulu kwa mdadisi ili kulenga na kutumia jukwaa lako.
Digi-ID ni bure kabisa! Hakuna ada, huduma za usajili, au gharama za matengenezo. Lakini gharama ni sehemu yake ya pili ya ubora wa Digi-ID. Kipengele chake cha msingi ni kwamba, kulingana na kipaumbele cha usalama wa DigiByte, Digi-ID ni njia salama zaidi, lakini rahisi kupatikana kwa tovuti, programu na zaidi.
Tovuti, programu au bidhaa hutoa nambari ya kipekee ya Digi-ID QR na kuiwasilisha.
Mtumiaji huchambua nambari ya QR kutoka kwa programu yoyote inayoungwa mkono na Digi-ID.
Mtumiaji huthibitisha ombi kwa kuingiza PIN yake au kwa ku-scan alama za vidole/uso wake.
Digi-ID hutuma ombi lililosainiwa kwa njia ya maandishi na mtumiaji atafanikiwa kuingia.
Sehemu nzuri ya kuanzia ni Digi-ID.io. Ikiwa unataka kujua zaidi juu ya maelezo na faida za Digi-ID, unaweza kurejelea mwongozo wa mtumiaji, mwongozo wa muuzaji na mwongozo wa ujumuishaji. Ikiwa unatafuta vifaa vya habari, tafadhali pata karatasi ya utangulizi na nembo.
Kwa kuwa Digi-ID ni chanzo wazi, kumbukumbu nyingi za kanuni zinaweza kupatikana kwenye GitHub kama vile DigiByte Core Development , Matthew Cornelisse na WHMCSSnow. Ikiwa unahitaji msaada zaidi tafadhali jiunge Watengenezaji wa programu za DigiByte kwenye Telegramu.
Kama wewe sio mtengeneza programu, unaweza kutaka kutumia suluhisho jumuisho lililo tayari za kwa tovuti yako au bidhaa. digiassetX hutoa programu-jalizi ya nodejs kwa ujumuishaji rahisi. Unaweza pia kutumia WordPress plugin kwa majukwaa ya WordPress.
Ndio! Digi-ID ni jukwaa linalokua haraka. Programu nyingi za uthibitisho na na pochi zinazoendana na Digi-ID zinapatikana katika sehemu ya Vipakuliwa.
Gundua huduma nyingine zinazoungwa mkono na Digi-ID ili kupata uthibitisho mzuri.
Makumi ya watu wa kujitolea kutoka ulimwenguni kote wamechangia DigiByte kwa njia mbalimbali kwa miaka kuifanya iwe kama ilivyo leo. Ni harakati ya kweli ya chini kwa chini. Tunakukaribisha kwa upendo ili ujiunge nasi!
Umoja wa DigiByte ni shirika la hisani la umma katika sehemu ya 501(c)(3) na hadhi ya hisani ya umma nchini Marekani. lengo lao ni kusaidia DigiByte kama mtandao wa blockchain wa kuaminika na usiopangwa kuhakikisha, kuhakikisha, kueleza, kujenga na kusambaza thamani kwa njia ya kuaminika na yenye ufanisi.
Jifunze zaidi - Wasiliana.
DGBAT ni mpango unaoratibiwa na jamii. Wanaongozwa na timu, ambayo washiriki wao husimamia timu kupitia mitandao ya kijamii, jamii, elimu, waandishi, na watengenezaji. Lengo ni kukuza DigiByte kupitia kampeni za elimu, ufikiaji na uuzaji.
Jifunze zaidi - Wasiliana.
Kila mtu anayefanya kazi kwenye DigiByte ni anajitolea bure bila malipo. Anza kuchangia maendeleo ya DGB leo au ujenge programu yako mwenyewe juu ya blockchain ya DigiByte.
Watengenezaji wa DigiByte kwenye Gitter.
Itifaki ya DigiByte Core kwenye GitHub.
Telegram ndio njia maarufu na rahisi ya kujishughulisha na jamii ya DigiByte ulimwenguni. Tafadhali jiunge na vikundi vilivyo chini ambavyo unavutiwa na au tazama orodha ya vikundi vyote vya DigiByte.
Taadhari Majadiliano Msaada Watengeneza programu Uchimbaji Uuzaji Uvumi Tafsiri
The DigiByte Wiki ni makala ya mtandaoni iliyojengwa na jamii Kwa ajili ya jamii. Ina data muhimu na mpya kama vile Mfumo wa DigiByte na jinsi ya kuongoza. Mtu yeyote anaweza kuchangia kwenye Wiki kwa kuunda akaunti ya bure ya mtumiaji na kuanza kuongeza habari kwenye DigiByte Wiki.
Onyo Epuka kujitangaza kusio na haya na viungo vya mialiko.
Jared Tate ndiye mwanzilishi na muundaji wa blockchain ya DigiByte. Jared alijitolea muda wake wote kwa ajili ya maendeleo ya DigiByte tangu Oktoba 2013. Amealikwa na MIT, Harvard na Capitol za Amerika kuzungumzia kuhusu teknolojia ya blockchain. Pia ni mwandishi wa kitabu cha Blockchain 2035 The Digital DNA of Internet 3.0, ambacho ni kitabu cha kwanza kilichoandikwa na mwanzilishi wa blockchain.
Kanusho la Mitandao ya Kijamii
Maoni, imani na maoni ya kibinafsi yaliyoonyeshwa na Jared Tate, Timu ya DigiByte Core, Muungano wa DigiByte & Timu ya Uhamasishaji ya DigiByte haionyeshi maoni ya kibinafsi, imani na maoni ya jamii.
Chagua programu kutuma, kukubali na kuhifadhi DigiBytes na DigiAssets zako au uthibitishe usalama kwa kutumia Digi-ID.
DigiByte Core ya sasa v7.17.3
DigiByte Core ina nakala kamili ya blockchain na inajenga uti wa mgongo wa mtandao. Mara nyingi hutumiwa na watengenezaji, masoko ya kubadilishana, na biashara nyingine, pamoja na wanachama wa jamii, kwa ajili ya kufanya mtandao kuwa wa kidecentrali kwa kuendesha node kamili. Pia inatumika kama mkoba wa programu.
DigiByte Core
Inapatikana kwa Windows, macOS, Linux & Snapcraft (64 Bit)
Onyo la Mkoba
DigiByte Core kama mkoba inapaswa kutumiwa na watumiaji wa juu tu ambao wanajua jinsi ya kuweka mkoba wao salama.
Ikiwa wewe si mtumiaji mwenye uzoefu, unaweza kutaka kutumia mkoba wa programu uliorahisishwa.
Unatafuta nyaraka zaidi? Ikiwa unahitaji habari ya msingi ya kifungu au habari ya kiufundi kwa mchakato wa ujumuishaji. Unaweza kufikia miongozo yote muhimu hapa chini.
Kanusho la Pochi
Pochi zote za zinazoletwa na makampuni mengine hapa zinashikiliwa na seva zao au stoo za programu husika. Hatutahusika na maswala yanayotokana na watoa huduma za pochi. Katika hali kama hiyo unapaswa kuwasiliana na huduma kwa wateja kutoka kwa hao wenye pochi.
Mitandao ya kijamii.
Fuatilia DigiByte kwenye majukwaa yote ya msingi ya kijamii ili upate habari mpya za DigiByte na ushiriki machapisho na marafiki zako kutusaidia kufanya sauti zetu zisikike kote ulimwenguni.